Home » » Polisi Tarime, Rorya wakamata jambazi na bunduki moja

Polisi Tarime, Rorya wakamata jambazi na bunduki moja

JESHI la polisi katika mkoa wa kipolisi wa Tarime na Rarya, limefanikiwa kumkamata mwanaume mmoja akiwa na bunduki moja aina ya Short Gun, pamoja na risasi nne akisubiri wenzake kutoka nchini Kenya, ili waweze kufanya ujambazi katika wilaya ya Tarime.

Aidha, jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata watu wanne wakiwa na noti bandia ambazo kama zingekuwa halali zingekuwa na thamani ya sh. milioni mbili na elfu 85.

Kaimu Kamanda wa polisi katika kanda ya polisi ya Tarime na Rorya, Bw. Simoni Mrashani, amethibitisha leo kuwepo kwa matukio yote mawili yaliyotokea jana katika maeneo na nyakati tofauti.

Kamanda Mrashani amesema kuwa katika tukio la kwanza polisi walifanikiwa kumtia mbaroni mwanaume mmoja, aliyetambuliwa kwa majina ya Mirango Chacha Mgaya (25), mkazi wa Nyerero wilayani hapa, akiwa na bunduki moja aina ya Short Gun ikiwa na risasi nne.

Amesema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatiwa katika eneo la sente ya Nyerero, na baada ya kupelekwa nyumbani kwake na kufanya upekuzi ndani ya nyumba yake, walimkuta akiwa na bunduki hiyo aliyokuwa ameifunika gunia na kuificha kwenye mto wa kitanda.

Ameongeza kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa juzi majira ya saa 10:30 jioni na kwamba baada ya kuhojiwa akiri na kusema kuwa alikuwa anasubiri wenzake kutoka nchini Kenya ili waweze kufanya uhalifu wilayani humo.

Amesema kuwa yeye alikuwa katika eneo hilo akifanya uchunguzi ili aweze kubaini mahali ambako wangevamia siku hiyo.

Na katka tukio jingine kamanda Mrashani amesema kuwa juzi usiku katika eneo la Rebu mjini Tarime, polisi walifanikiwa kukamata watu wanne wakiwa na noti bandia,  ambazo kama zingekuwa halali zingekuwa na thamani ya zaidi ya shilingi milini mbili na elfu 85.

Amesema kuwa pesa hizo zilikuwa niza shilingi elfu kumikumi ambazo ni milioni mbili na elfu tanotano shilingi 85,000 na kwamba walikuwa wanataka kwenda kununua mawe ya dhabu mgoni kwa kutumia fedha hizo bandia.

Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni pamoja na Martin Chacha Matima (60), mkazi wa kijiji cha Nyangoto Nyamongo, Zakaria Michael (33), Mathias Peter (32) na John Chacha (60), ambao wote ni wakazi wa Rebu mjini Tarime.


Amesema kuwa kukamatwa kwa watuhumiwa hao kumetokana na taarifa za siri kutoka kwa raia wema na kuongeza kuwa watafikishwa mahakamani wakati wowote baada ya upelelezi wa polisi kuwa umekamilika.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa