Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mara, kimeomba radhi kwa chama
cha waandishi wa habari mkoani humo (MRPC) kutokana na kitendo
kilichofanywa na wafuasi wa chama hicho tawala, kwa kumpiga mwandishi wa
habari wa gazeti hili na kusema kuwa waliohusika watachukuliwa hatua.
Mwenyekiti wa CCM mkoani Mara, Christopher Sanya,
alisema wanaomba radhi kwa mwandishi huyo, Christopher Maregesi pamoja
na kwa waandishi wote wa habari wa Mkoa wa Mara.
“Mimi kwa niaba ya chama ninaomba radhi kwa
kitendo alichofanyiwa….ninakikemea kwani si cha kiungwana,”alisema Sanya
na kuongeza: “Tutafanya uchunguzi na wale watakaobainika kuhusika
tutawachukulia hatua.”
Aliongeza: “CCM tunathamini mchango wa waandishi wote kwa ujumla, hivyo kitendo kilichofanywa si cha kiungwana.”
Maregesi alishambuliwa Februari 8 mwaka huu na
wafuasi wa CCM mjini Bunda, muda mfupi baada ya kumalizika kwa mkutano
wa kampeni wa kumnadi mgombea wa udiwani wa chama hicho katika Kata ya
Nyasura.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment