Home » » CWT Bunda yawashangaa wabunge wa bunge la katiba

CWT Bunda yawashangaa wabunge wa bunge la katiba

CHAMA cha walimu (CWT) katika wilaya ya Bunda, mkoani Mara, kimesema kuwa iwapo walimu hawatalipwa madai yao mbalimbali ifikapo mwishoni mwa mwezi huu wataanza mgomo.

Hayo yamesema na mwenyekiti wa chama hicho wilayani Bunda, Bw. Francis Ruhumbika, kwenye mkutano mkuu maalumu wa chama hicho, uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha ualimu Bunda.

Bw. Ruhumbika amesema kuwa walimu wilayani Bunda, wanaidai serikali zaidi ya shilingi bilioni 2.1 ambazo ni za madai mbalimbali yaliyohakikiwa na yasiyohakikiwa na kwamba uhakiki huo ulifanyika mwezi oktoba mwaka jana.

Amesema kuwa kwa vile baraza kuu la CWT taifa, limeshatangaza mgogoro na serikali kuhusu madai mbalimbali ya walimu, walimu wote wilayani Bunda watagoma kuingia madarasani iwapo hawatalipwa fedha zao.

Akizungumzia posho ya wabunge maalumu la katiba, kwa kudai waongezee posho kwamba ya sh. laki tatu kwa siku ni ndogo, mwenyekiti huyo wa CWT Bunda, amewashanga sana wajumbe hao na kusema kuwa kiasi hicho ni kikubwa mno.

Amesema kuwa kama  wajumbe hao hawataki ni bora wakarudi majumbani mwao na Rais ateuwe wengine wanaoweza kufanya kazi hiyo kwa maslahi ya umma hata kwa posho ya shilingi 40,000 kwa siku.

Amesema kuwa kiasi cha shilingi laki tatu kwa siku ni kikubwa mno na kuongeza kuwa kiasi hicho ni sawa na mshahara wa mtu anaopata kwa mwezi mmoja na kwamba wapo walimu ambao wanalipwa mshahara  wa mwezi chini ya hiyo shilingi laki tatu.

Aidha, CWT wilayani Bunda, kimeliomba Bunge maalumu la  katiba kuweka kipengere katika katiba mpya kwamba mgomo uwe ni haki ya wafanyakazi.

Akijibu riasala ya walimu hao mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Bunda, Bw. Simoni Mayeye, amesema kuwa changamoto zinazowakabili walimu ni nyingi na kwamba atashirikiana na CWT kadiri ya uwezo wake katika kutatua ufumbuzi wa changamoto hizo.

Bw. Mayeye amesema kuwa madai mbalimbali ya walimu yaliyohakikiwa yaliwasilishwa ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma.


Amesema kuwa yeye kama mwajiri hapendi hali hiyo itokee katika halmashauri yake na kuongeza kuwa kuwahi au kuchelewa kwa marekebisho ya mishahara, kulipwa mapunjo na kupandishwa madaraja hutokana na sababu mbalimbali.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa