Home » » OFISA KILIMO RORYA AFIKISHWA KOTINI KWA RUSHWA 20,000.

OFISA KILIMO RORYA AFIKISHWA KOTINI KWA RUSHWA 20,000.

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Mara imemfikisha katika Mahakama ya Wilaya ya Tarime Bw.Emmanuel Samwel Kambenga ambaye ni Afisa kilimo na Mwajiri wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya  kwa kosa la kudai rushwa ya shilingi elfu ishirini na kumfungulia kesi ya Jinai yenye namba 35 ya mwaka 2014.

Kesi imefikishwa Mahakamani hapo na mwendesha mashitaka wa Taasisi hiyo Wakili Erick Kiwia februari 4,mwaka huu ambapo mpaka sasa ipo mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Tarime Adrian  Kilimi ambapo anakosa la kudai rushwa ya shilingi elfu ishirini(20,000) kutoka kwa mkulima wa kijiji cha Randa kilichopo wilayani Rorya ambaye(jina limehifadhiwa).

Katika kutekeleza majukumu yake hayo Ofisa huyo alifika kwenye shamba la mkulima huyo  na kukagua uharibifu uliokuwa umefanywa,kisha akaandaa tathmini ya uharibifu uliofanywa na mifugo hiyo katika shamba hilo baada ya kukamilisha tathmini alikataa kuikabidhi kwa mkulima taarifa hiyo akidai apewe rushwa ya shilingi elfu ishirini ,na kuwa  bila fedha hiyo asingempatia mkulima huyo taarifa ya tathmini.

Mshitakiwa alikana mashitaka hayo na yuko nje kwa dhamana na kesi hiyo itaendelea mahakamani hapo March 5,mwaka huu, aidha Taasisi hiyo inatoa wito kwa wakulima na wafugaji kuiga mfano wa mkulima huyo wa kijiji cha Randa wa kudai haki kwa misingi ya sharia.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa