KUSITA
kwa utekelezaji kwa maamuzi ya mahakama kwa baadhi ya vyombo vya
Dora imekuwa ni kikwazo kikubwa katika ufanisi wa mahakama na hivyo
wananchi kutokuwa na imani na Mahakama jambo linalotishia amani na
kuthoofisha utawala wa sheria.
Akisoma Hotuba yake jana Katika siku ya mahadhimisho ya Sheria Nchini Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Tarime Adrian Kilimi amesema Serikali kupitaia vyombo vyake vya Dora vya polisi, Magereza na Uhamiaji ndiyo vinawajibu wa kuwaleta watuhumiwa Mahakamani pamoja na kuhakikisha upelelezi wa kesi za watu unakamilika kwa wakati lakini imekuwa ni tatizo kutozingatia muda unaotakiwa.
Kilimi alieleza changamoto Nyingine inayoikabili Mahakama kuwa ni kukosekana kwa mashahidi inasababisha kutomaliza kwa wakati kesi za watu matokeo yake wananchi kufikili Mahakama haitendi haki na kusababisha uvunjifu wa amani ambapo pia ukosefu wa vitendea kazi imekuwa ni changamoto katika Mahakama za Wilayani Tarime.
Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tarime John Henjewele aliyekuwa mgeni Rasmi kwenye sherehe hizo aliomba kunapofanyika mahadhimisho ya sheria basi mahabusu walioko gerezani washiriki kwenye sherehe kwakuwa siku hiyo ni muhimu kwao kuweza kujifunza maswala mbalimbali ya kisheria.

0 comments:
Post a Comment