Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Tarime/Rorya, Kamishina Msaidizi, Justus Kamugisha.
Watu hao, ambao kwa sasa wanaendelea kuhojiwa, walikamatwa kufuatia msako mkali unaofanya na askari wa jeshi hilo kwa kushirikiana na wananchi.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Tarime/Rorya, Kamishina Msaidizi, Justus Kamugisha, alisema watu hao walikamatwa tangu kuanza kwa msako huo Januari 26, mwaka huu.
Alisema msako huo unaendelea na kusisitiza kuomba ushirikiano wa taarifa kutoka kwa wananchi.
“Kuanzia usiku wa Januari 25-27 alikuwa akionekana mtuhumiwa mmoja wa ujambazi asiyefahamika. Alikuwa akitekeleza mauaji kwa kutumia silaha aina ya SMG au SAR kutokana na maganda ya risasi yaliyopatikana maeneo ya matukio mawili.
Kwa sasa imeonekana kwamba, wahalifu wa makosa ya unyang'anyi wa kutumia silaha za moto ni zaidi ya watu watano,” alisema Kamishna Kamugisha.
Alisema watuhumiwa 10 waliokamatwa majina yao yanahifadhiwa kwa ajili ya uchunguzi ili kuwapata wanaoshirikiana katika uhalifu na kwamba, wanawahoji kabla ya kuwafikisha mahakamani.
Aliwaonya wanasiasa wanaojaribu kuingilia operesheni hiyo kwa kutaka kuwatetea wahalifu, huku Jamii ikiwataja watuhumiwa kuhusika katika vitendo vya mauaji na unyang'anyi kwa raia wasio na hatia.
Aliwataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa kwa vyombo vya dola ili watuhumiwa wakamatwe na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment