Home » » WAKULIMA WA CHAI WAELEZA CHANGAMOTO

WAKULIMA WA CHAI WAELEZA CHANGAMOTO

BEI ndogo ya zao  la chai na kutotolewa kwa malipo kwa wakati  kwa wakulima wa chai kutoka kwa wawekezaji ni changamoto kubwa inayosababisha wananchi wakiwamo wa wilaya  ya Tarime kutojitokeza kulima chai kutokana na zao hilo kutowanaufaisha wakulima.

Hayo  yameelezwa na wadau wa kilimo cha chai Kanda ya Ziwa wakati wa semina yao ya kujadili changamoto zinazowakabili wakulima na namna  ya kuboresha zao la chai iliyofanyika katika ukumbi wa Hotel  Godland Wilayani Tarime.

Wakulima Wilayani Tarime Walisema kuwa  zao la chai limeanza kulimwa katika Wilaya hiyo 2002 nakwamba bei ya 206 kwa kilo moja ya majani mabichi ya chai na gharama za pembe jeo ni sababu kubwa inayowafanya  watu kutozidi kujitokeza  kulima zao la chai.

Kwa Upande wa wakulima wa zao la Chai Mkoani Kagera wao wameomba kufukuzwa kwa Mwekezajiwanaomba kufukuzwa kwa mwekezaji wa Kampuni ya chai kwa kile walichoeleza kuwa ana mahusiano na majibu mabaya kwa wakulima na halipi fedha kwa wakati pindi anapouziwa chai.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa