MGODI wa North Mara Barrick na Migodi mingine ya wachimbaji wadogowadogo imedaiwa ni sababu ya utoro kwa wanafunzi wa shule ya msingi Nyabusara katika Kijiji cha Murito iliyoko Nyamongo Wilayani Tarime kutokana na wanafunzi kutofika shuleni nakwenda kujishughulisha na shughuli za mgodini.
Shughuli hizo ni pamoja na kwenda kuokota mawe ya dhahabu huku wengine wakibaki nyumbani kulea watoto pindi wazazi waendapo migodini kutafuta riziki.
Hali hiyo ya wanafunzi kutofika shuleni imesababisha kushuka kwa kiwango cha taalamu shuleni hapo ambapo kwa matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka jana shule ya msingi Nyabusara ilishika na fasi ya tisa katika shule dhahifu zilizofanya vibaya katika mtihani wa kumaliza darasa la saba kati ya shule 134 Wilayani Tarime.
Hayo yameeelezwa na Mwalimu mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Nyabusara Sharifa Mchili na kwamba kuna haja ya wazazi kudhibiti watoto kufika shuleni kwani walimu wanapowaadhibu wanafunzi kwa utoro wazazi wamekuwa wakilalamika na kusababisha kutokuwepo kwa mahusiano mazuri kati ya wazazi na walimu.
Mwenyekiti wa Kijiji Cha Murito Joseph Mangure amesema kuwa Serikali ya kijiji Kupitia Vitongoji vyake tayali imepanga mikakati kuhakikisha watoto wanafika shuleni na kuhudhulia vipindi darasani kwa kile alichoeleza kuwa mtoto atakayeonekana hajafika shuleni Mzazi atawajibika, na akawataka walimu kutoa taarifa ya majina kwa wanafunzi ambao hawatafika shuleni.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment