Home » » Ukosefu wa vyoo: walimu walazimika kurudi majumbani kujisaidia

Ukosefu wa vyoo: walimu walazimika kurudi majumbani kujisaidia

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
WALIMU wa shule ya Msingi Mapinduzi'A'katika wilaya ya Serengeti Mkoani Mara wanalazimika kurudi majumbani kwao kujisaidia kutokana na shule hiyo kutokuwa na choo kwa zaidi ya mwaka,hali inayopelekea muda mwingi wa vipindi kupotea.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Jamse Johannes amesema walikuwa wanatumia choo cha kanisa la Sayuni na baada ya kuweka uzio,walimu wanalazimika kurudi kwenye mijji yao ama kwa majilani kujisaidia,hali ambayo inawadhalilisha ikizingatiwa hiyo ni shule ya mjini.

Amesema tatizo hilo limeishawasilishwa ngazi ya wilaya,lakini hakuna ufumbuzi wa kuwawezesha walimu kushiriki vema kwenye vipindi, kwa kuwa muda unaopotea kwa kurudi majumbani kwao una athari kubwa kwa watoto kitaaluma.

Mwenyekiti wa Mtaa wa NHC, Bw,Elias Nyamraba amesema mbali na walimu kukosa choo ,pia choo cha wanafunzi kiko katika eneo la mtu ambaye ameishatoa notisi kwa kuwa anataka kuendeleza eneo lake,ikifikia hatua hiyo huenda shule ikafungwa.

Ofisa elimu wilaya hiyo William Mabanga amekiri kuwepo kwa tatizo hilo,na kusema karibu shule zote wilayani hapo hazina vyoo vya walimu,kwa kuwa mkazo uliwekwa kujenga vyoo vya wanafunzi,na kuahidi kuwa watatoa kipaumbele ili kuwaondoa adha walimu hao.

Mwenyekiti wa kamati ya Elimu ,afya na maji ya baraza la madiwani ,Bw.Daniel Kegocha amesema ametembelea shule hiyo baada ya kufuatwa na walimu na kuona hali halisi na kuahidi kuwasilisha baraza la madiwani kwa hatua zaidi.

Shule hiyo ina walimu 37 wakike wakiwa 31 na wakiume 6 na wanafunzi 890.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa