Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
SERIKALI imeombwa kuchangia Madawati katika shule ya msingi
Nyabusara na Murito zilizopo Nyamongo Wilayani Tarime Mkoani Mara ili
kuwapunguzia mzigo wananchi wa kijiji cha Murito kwakuwa wananchi hao
wamekuwa wakijitolea kuchangia manedeleo ya kijiji ukiwamo ujenzi wa shule.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Murito Joseph Mangure amesema
kuwa licha ya kijiji hicho kuwa Nyamongo hakipo kwenye utaraitibu wa
kuwezeshwa na Mgodi wa Nort Mara lakini wananchi
wamekuwa na mwitikio wa kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo zikiwamo za
ujenzi wa nyumba 7 za walimu na madarasa nne shule ya msingi Murito.
Mwalimu Mkuu msaidizi wa shule ya msingi
Nyabusara Sharifu Mchili amesema kuwa shule hiyo ina idadi ya wanafunzi 696 na
ina upungufu mkubwa wa madawati ambapo kila darasa lina madawati 6 pekee
wakati darasa la chekechea likiwa halina dawati hata moja na hivyo kusababisha
wanafunzi kutosoma vizuri na walimu kupata wakati mgumu wakati wa ufundishaji.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Athuman
Akalama amesema kuwa anatambua mchango wa wananchi katika uchangiaji wa
maendeleo lakini halmashauri inashindwa kutatua matatizo yote kutokana na wingi
wa shule za msingi 101 zote zikiwa na mahitaji mengi huku Serikali nayo
ikitoa pesa kidogo kulingana na maombi ya Halmashauri nakusababisha kuwepo kwa
malalamiko mengi ya wananchi.
0 comments:
Post a Comment