Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mvua zinazoendelea
kunyesha katika Mikoa mbalimbali hapa Nchini zinazidi kusababuisha athari ikiwa
ni pamoja na uharibifu wa Mazao, kubomolewa kwa Nyumba suala ambalo linazidi kuwapa
Watanzania changamoto.
Katika wilaya ya Rorya
Mkoani Mara katiya kata Tano ambazo ni Bukura, Ikoma,Nyahongo,Nyamagaro,na
Korio(Utegi) zimekumba na Maafa makubwa ambayo
yamesababishwa na Mvua zinazoendelea kunyesha nyumba 297 zikiwemo za bati160 na
Nyasi137 zimekumbwa na maafa hayo katika kata hizo.
Katika Taasisi za
Serikali Jengo moja sekondari ya Nyanduga bweni la wavulanalimeezuliwa bati na
shule mbili ya Msingi,Ofisi moja ya Ofisa Mtendaji wa kata ikiwa ni pamoja na
Chuo cha Uvuvi kilichopo Shirati Nyancha Taarafa ya Nyamigaro kimetolewa paa
katika jengo la kujivunzia jinsi ya kubamba ngozi pamoja na kituo cha Afya
Utegi jengo moja limeweza kutikiswa na Upepo huo.
Aidha katika kutoa
taarifa Mkuu wa Wilaya ya Rorya Bw: Elias Goroi amesema kuwa baada ya Kuzunguka
na kamati ya Maafa Wilaya wamebaini kuwa Wananchi wanamahitaji ya Chakula kwani Ekali 910za mazao mbalimbali kama
vile Mtama , Mahindi na Migomba zilweza kuhalibiwa na Mvua ya Mawe iliyonyesha
ususani katika kata ya Ikoma.
Hata hivyo Mkuu wa
wilaya huyo amesema kuwa Kamati ya Maafa imeona kuwa kuna Mahitaji ya Chakula Tani 12 Tani 2 za Mtama
na Tani 2 za Mahindi ambapo zitasaidia kulisha Watu kwa Mda mfupi
Sanjari na hayo mkuu wa
Wilaya ameongeza kuwa amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo aweze kusambaza Madawa katika Vijiji vilivyoathilika kwa ajili ya Taadhali ya Milipuko ya Magonjwa
ambaya yanaweza kulipuka uku ikiwa zikigawiwa Chandarua 120 kwa akina Mama
wajawazito na watoto
Mwisho mkuu wa Wilaya
huyo ametoa Mwito kwa jamii kuwa Waweze kujenga Nyumba imara kwa lengo la kulinda Usalama wao uku akisema katika
Tathimini iliyofanywa hakuna Vifo
vilivyotokea kulingana na maafa hayo.
0 comments:
Post a Comment