Home » » CHANGAMOTO ZINAZO IKABILI IDARA YA ELIMU BUNDA

CHANGAMOTO ZINAZO IKABILI IDARA YA ELIMU BUNDA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

IDARA ya elimu katika wilaya ya Bunda mkoani Mara, inakabiliwa na vchangamoto nyingi, ikiwa ni pamoja na migogoro ya mipaka ya maeneo ya shule, utoro wa wanafunzi na walimu, pamoja na kitengo cha ukaguzi kukosa chombo cha usafiri.

Hayo yamebainishwa jana katika mkutano wa kuboresha elimu wilayani Bunda, uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha ualimu Bunda, kilichoko mjini hapa.

Afisa elimu wa shule za msingi wilayani hapa , Bw. Jeshi Lupembe, amesema kuwa kunaupungufu mkubwa wa walimu wapatao 236 na kwamba katika mgao wa walimu wapya, wamefanikiwa kupata walimu 86 tu, huku wanaostaafu mwaka huu wakiwa ni 65 na kwamba tatizo hilo linabakia kuwa pale pale.

Bw. Lupembe amesema kuwa changamoto nyingine ni mwamko duni wa wazazi na waliezi kuchangamkia elimu, kwani baadhi yao hawafuatili mienendo ya masomo ya watoto wao.

Ameongeza kuwa nyingine ni ukosefu wa usafirili kwa ajili ya ukaguzi kwa sababu gari liliopo ni bovu, kutokuwepo usimamizi wa mara kwa mara na ukosefu wa chakula cha wanafunzi kwa baadhi ya shule.

Kwa upande wake afisa elimu wa shule za sekondari wilayani hapa, Bw. Martin Nkwabi, amesema kuwa changamoto kubwa ni upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi, hali ambayo imekuwa ikisababisha wanafunzi kutokufanya vizuri katika masomo hayo.

Bw. Nkwabi amesema kuwa pamoja na kuwa na upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi 158, lakini katika mgao wa walimu wapya wamefanikiwa kupata walimu 15 tu, wa somo hilo na kwamba hadi sasa walioripoti ni wanane.

Aidha ameongeza kuwa changamoto nyingine ni upungufu wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia, ikiwa ni pamoja na vitabu vya maabara na madawa na nyenzo nyinginezo.

Naye Naibu mkaguzi mkuu wa shule za msingi wilayani hapa, Bi. Anna Ouma, amesema kuwa kitengo hicho kinakabiliwa na changamoto nyingi, ambazo inatakiwa zipatiwe ufumbuzi haraka, ili kuinua kiwango cha elimu wilayani hapa.

Mkutano huo wa kuboresha hali ya elimu wilayani Bunda , ulishirikisha wadau mbalimbali, wakiwemo TSD, Ukaguzi, Walimu wakuuu wa shule za msingi, Waratibu elimu Kata, Wakuu wa shule za sekondari, Idara ya elimu msingi na Idara ya elimu sekondari.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa