Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
UELEWA mdogo wa jamii ni chanzo cha biashara
duni ya Utalii wilaya ya Serengeti Mkoani Mara ambayo inazungukwa na
asilimia 70 ya eneo la hifadhi na mapori ya akiba.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo John Ng’oina amesema hayo wakati anafungua semina ya wadau kwenye ukumbi wa Maktaba mjini Mugumu kujadili namna ya kuinua biashara hiyo,na kuwataka wazazi kuwasomesha watoto wao,kwa kuwa elimu ndiyo itafanya mapinduzi ya kimitizamo.
Mshauri wa Matumizi bora ya Maliasili wilaya hiyo kupitia Mpango wa shirika la Maendeleo la Kijermani Bw,Bennie Bloemberg amesema fursa hiyo inapaswa kujibu changamoto za jamii kiuchumi kama itatumiwa vizuri.
Amesema kupitia mpango huo wanataraji kuunda bodi ya Utalii ya wilaya,kuandaa fursa zilizomo na kuzitangaza ili kuwawezesha wageni kuja kuwekeza,na kufungua fursa kwa wananchi Ili waweze kunufaika kiuchumi.
Hata hivyo baadhi ya washiriki wameomba serikali kuhakikisha barabara ya lami inajengwa ambayo itasaidia kufungua fursa nyingi za kiuchumi na kuwawezesha watu kuleta bidhaa kwa gharama nafuu.
0 comments:
Post a Comment