Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MAHABUSU katika Gereza
la Wilaya ya Tarime Mkoani Mara leo asubuhi ameonekana akiwa juu ya Mti ulio ndani ya gereza akipiga yowe na kuomba
wanaharakati,Waandishi wa habari na Haki za Binadamu wamsaidie baada ya kuchelewa
kwa kesi yake inayomkabili ya mauwaji ya mwaka 2010.
Mahabusu huyo akisikika
kwa sauti alilalamika kuwa tangu akamatwe mwaka 2010 kwa kukabiliwa na kesi ya
mauwaji hadi sasa kesi yake inaendelea kupigwa chenga bila kushughulikiwa na
kuzidi kusota gerezani.
Mahabusu huyo alipiga yowe akiwataka wanaharakati,Haki za
Binadamu na akawaomba waandishi wa habari waandike malalamiko yake huwenda
Serikali itamsaidia ili kesi yake ikamilike kwa madai kuwa kesi yake inapigwa
tarehe na amechoka kuishi gerezani
bila matumaini ya hatima ya kesi yake.
Mkuu wa Wilaya ya Tarime
John Henjewele alisema kuwa
amepokea taarifa ya mahabusu huyo kulalamika juu ya mti juu ya kucheleweshwa
kwa kesi yake na kuahidi kufatilia kwakuwa yuko kikazi Kata ya Nyamwaga Wilayani Tarime.
0 comments:
Post a Comment