Home » » DASP YATOA MIL. 17.4 MRADI WA UFUGAJI SAMAKI TARIME

DASP YATOA MIL. 17.4 MRADI WA UFUGAJI SAMAKI TARIME

VIJIJI sita Wilayani Tarime vinatarajia kunufaika na mradi wa ufugaji wa samaki kwa njia ya malambo ambapo mradi wa uwekezaji katika kilimo (DASP) umetoa mili.17.4 ili kuwawezesha wafugaji wa samaki.

 Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime ambaye pia ni Ofisa kilimo Syrvanus Gwiboha. Amesema kuwa fedha hizo zimetolewa kwa vijiji vya Gibaso,Itiryo,Nyamirambaro,Nkerege,Weigita,na Kitawasi.

Gwiboha amesema kuwa fedha hizo zimetolewa  kwa ajili ya ununuzi wa vifaranga,Chakula bora cha samaki,Nyavu za kuvulia samaki na kila lambo litaghalimu milioni 2 na laki 9.


Ameongeza kuuwa lengo la kutolewa  kwa fedha hizo ni kuwapunguzia bei ya samaki kwakuwa kutakapokuwapo na malambo mengi samaki watanunuliwa kwa wingi tena kwa bei nafuu tofauti na sasa ambapo samaki wa Ziwa Victoria mmoja anauzwa kuanzia sh.3000-5000.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa