Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MAHAKAMA ya Wilaya ya Musoma, mkoani Mara, imemhukumu kifungo cha
miaka 30 jela pamoja na kuchapwa viboko 10, mkazi wa Mtakuja, Makarani
Wambura (25) baada ya kupatikana na hatia ya unyang’anyi wa kutumia
silaha.
Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Karim Mushi,
baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa
mashitaka.
Hakimu Mushi, alisema ameridhika pasipokuacha shaka na ushahidi
huo, hivyo kumhukumu Wambura kifungo cha miaka 30 jela, pamoja na
kuchapwa viboko 10 wakati akiingia gerezani.
Awali, Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Jonas Kaijage, alidai
Septemba 29 mwaka jana, saa 6 usiku, katika baa ya Simba Club, iliyoko
katika Mtaa wa Mtakuja mjini Musoma, mshitakiwa akiwa na wenzake
watano ambao walitoroka, walivamia baa hiyo na kufanikiwa kuiba pesa
taslimu sh 350,000 na vitu mbalimbali vyenye thamani ya sh 900,000,
mali ya Martha Gikaro, mkazi wa mtaa huo.
Alidai kabla ya kufanya unyang’anyi, walitumia silaha mbalimbali za
jadi yakiwemo mapanga na marungu ili kufanikisha kitendo hicho.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment