Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WANANCHI wa Wilaya ya Butiama mkoani Mara, wametakiwa kujitokeza
kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la kupiga kura ili
uchaguzi utakapofika waweze kupata haki yao ya msingi ya kuwachagua
viongozi wanaowataka.
Kauli hiyo imetolewa na mjumbe wa Kamati Tendaji ya Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilaya ya Butiama, Yusufu Kazi,
wakati akiwashukuru wajumbe kwa kumuamini na kumpa kura nyingi kwenye
uchaguzi wa mkutano mkuu wa Jimbo uliofanyika hivi karibuni.
Kazi, alisema wananchi wote wanatakiwa kwenda kujiandikisha kwenye
daftari hilo zoezi litakapoanza, kwani bila kujiandikisha watakosa haki
yao ya msingi ya kuwachagua viongozi wanaowataka kwa ajili ya
maendeleo yao.
Pamoja na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye
daftari hilo, alitoa shukrani kwa Rais Jakaya Kikwete kwa kuwapa
Wilaya Butiama.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment