Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WANANCHI wa Kata ya Kukilango, Mkoa wa Mara wamemtaka Mjumbe wa kamati tendaji ya chama cha Demokrasi na maendeleo (CHADEMA), Yusuph Kazi, kugombea Ubunge katika uchaguzi Mkuu mwaka 2015.
Wananchi hao, waliyasema hayo jana katika sherehe za kumkaribisha Mjumbe huyo baada ya kushinda nafasi hiyo katika uchaguzi wa chama hicho uliofanyika hivi.
Walisema kuwa wako tayari kumpa nafasi hiyo endapo atachukua fomu ya kugombea ubunge Musoma vijijini.
Aidha, walisema kuwa hatua hiyo imetokana na mbunge wao wa sasa Nimrod Mkono (CCM) kutowashirikisha katika mambo ya maendeleo.
Diwani wa kata hiyo, Ihunyo Issa, aliwataka wananchi hao kumpa ushirikiano mjumbe huyo ili kuhakikisha anaipatia maendeleo kata hiyo.
Kazi alipoulizwa kuhusiana na maombi ya kugombea ubunge alikiri kukubali na kuahidi kuendelea kutatua matatizo ya.
0 comments:
Post a Comment