Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkoa wa Mara ni kati ya mikoa 30 ya Tanzania. Musoma ndipo makao makuu ya mkoa.
Mara imepakana na mikoa jirani yaMwanza na Shinyanga upande wa kusini, Arusha upande wa kusini-mashariki, Kagera kwa njia ya Ziwa Nyanza (au Viktoria) na Kenya upande wa mashariki.
Idadi ya wakazi ni 1,368,602 (2002). Makabila ni mengi kuliko mikoa yote ya Tanzania, kama vile Waluo, Wajita, Waruri, Wazanaki, Wakuria, Wakabwa, Wakiroba, Wasimbiti, Wangoreme, Wakwaya, Waikoma, Wanata, Waisenye, Waikizu, Wasizaki, Wasukuma and Wataturu.
Kuna wilaya za Bunda, Serengeti, Tarime, Rorya, Butiama, Musoma mjini na Musoma vijijini.
Sehemu kubwa ya Hifadhi ya Wanyama ya Serengeti iko ndani ya Mkoa wa Mara.
0 comments:
Post a Comment