Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WAKULIMA wa mahindi wilayani Tarime katika mkoa wa Mara, wameuomba
uongozi wa wilaya hiyo kusaidia kuwadhibiti watumishi wakiwamo maofisa
wa Kilimo katika tarafa ya Inchugu, ambao wamekuwa kero kwa kuwakamata
wakiwa na mazao yao wanapokwenda kuyauza katika masoko ya ndani na nje
ya wilaya hiyo.
Akizungumza na gazeti hili, Diwani wa Kata ya Pemba, Serenga Wangwe
alisema kwa sasa wilayani hapa kuna mavuno ya mazao yakiwemo mahindi, na
wakulima wakitaka kwenda kuyauza mjini Tarime ama nje ya wilaya hiyo
wamekuwa wakisumbuliwa kwa kukamatwa na baadhi ya watumishi wa Serikali
wakiwemo wa Idara ya Kilimo Kituo cha Sirari huku watumishi hao
wakioneshwa vielelezo na barua za kutoka vijijini.
Alisema hali hiyo inawafanya wakulima kushindwa kwenda kuuza mazao
yao kwa bei ambayo ingewainua na kuyauza kwa walanguzi kwa kupewa bei ya
chini kwa gunia moja la kilo 108 kwa Sh 50,000, huku walanguzi nao
wanaodai wana vibali vya kusafirisha mahindi, wanakwenda kuyauza
wilayani Sh 56,000.
CHANZO ; HABARI LEO.
0 comments:
Post a Comment