Home » » PROP. MAGEMBE AAGIZA NG'OMBE WALIOKAMATWA SERENGETI KUACHIWA.

PROP. MAGEMBE AAGIZA NG'OMBE WALIOKAMATWA SERENGETI KUACHIWA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.  
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof.  Jumanne Maghembe, amewaagiza wafanyakazi wa Hifadhi ya Serengeti kuachia zaidi ya ng’ombe 6,000 waliokamatwa kwenye hifadhi hiyo.
 
Waziri huyo alitoa agizo hilo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Busega (CCM), Raphael Chegeni, bungeni jana.
 
Chegeni alisema utalii ili uweze kuendelea kunatakiwa ushirikishwaji wananchi wanaoishi kandokando ya hifadhi hifadhi pamoja na kuwapo kwa mahusiano mema.
Alisema kuna mgogoro baada ya zaidi ya ng’ombe 5,000 wa wafugaji wa vijiji vya Kigirisi na Nyamikoma katika Jimbo la Busega kukamatwa na askari wa hifadhi hiyo.
 
Alisema mifugo hiyo imefungiwa kwenye pori kwa zaidi ya siku tatu ili wafugaji hao walipe faini.
 
“Kama kweli tunataka uhifadhi mzuri wa ushirikishwaji, serikali inachukua hatua gani kuruhusu mifugo iliyokamatwa kuachiwa kwa kuwa imeingizwa kwenye hifadhi kinyume cha utaratibu,” alisema.
 
Akijibu, Prof. Maghembe alisema wafugaji wa vijiji vinavyopakana na hifadhi ya Serengeti wameingiza ng’ombe zaidi ya 6,000 ambao wamekamatwa na askari wa hifadhi hiyo kwasababu ni kinyume cha sheria.
Hata hivyo, alisema juzi usiku alitoa agizo la kuachiwa ng’ombe hao na tayari wanavijiji wameanza kuchukua mifugo yao.
 
Awali, katika swali la msingi, Mbunge wa Viti Maalum, Risala Kabongo (Chadema), alitaka kujua mpango wa serikali wa kuongeza idadi ya wageni katika hifadhi za mikoa ya Kusini za Ruaha, Kitulo, Udzungwa, Mikumi na Katavi na maeneo mengine ya kihistoria.
 
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ramao Makani, alisema wizara hiyo kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na Shirika la Misaada la Marekani (USAID), ilifanya upembuzi yakinifu na kuandaa mikakati ya kuendeleza na kutangaza utalii wa eneo la Kusini mwa Tanzania 2015.
 
Alisema ili kutekeleza mikakati hiyo serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia itatekeleza mradi utakaojulikana kama Tanzania Resilient Natural Resources Management For Growth Project” ambao utatekelezwa kwa miaka sita na utaanza kutekelezwa Januari, 2017 na kugharimu takriban Marekani milioni 100.
 
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa