Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
DAR ES SALAAM
Mkuu
wa Wilaya ya Rorya Mhe. Felix Lyaniva ametoa wito kwa wanarorya
wanaoishi Jijini Dar es salaam kuwekeza kwenye fursa zilizopo katika
wilaya hiyo iliyopo mkoani Mara.
Ameyasema
hayo leo Jijini Dar es salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari
kuhusu mkutano wa wanarorya wanaoishi Da es salaam utakaofanyika katika
ukumbi wa Karimjee siku ya jumapili Februari 17, 2016 kuanzia saa nane mchana.
“Wilaya
yetu ya Rorya ina fursa nyingi za uwekezaji zikiwemo za biashara, ardhi
yenye rutuba, gesi asilia, mifugo pamoja na misitu, lakini pamoja na
kuwa na fursa za rasilimali zote hizo bado ni miongoni mwa wilaya ambazo
ziko nyuma kimaendeleo hivyo tunahitaji wanarorya wachukue hatua”
alisema Mhe. Lyaniva.
Mhe. Lyaniva ameongeza kuwa licha ya wilaya ya Rorya kupiga hatua na kuwa Halmashauri haijawa na kasi ya kuridhisha kutokana
na wanarorya waishio nje ya wilaya hiyo kutoshiriki ipasavyo kwenye
fursa za kiuchumi na kwenye utatuzi wa changamoto mbalimbali
zinazoikabili wilaya hiyo.
Aidha,
Mhe. Lyaniva ameelezea baadhi ya changamoto zinazowakumba wananchi wa
Rorya zikiwemo za ugonjwa wa Ukimwi, njaa pamoja na ukosefu wa huduma
bora za kijamii kama vile maji safi na salama, barabara, Hospitali,
shule, vyuo vya ufundi pamoja na vituo vya kutosha vya ulinzi na usalama
kwa upande wa Jeshi la Polisi.
Kabla ya mwaka 2007 Rorya ilikua sehemu ya Wilaya ya Tarime, kwa sasa Rorya imekua wilaya mojawapo kati ya wilaya nne zilizopo Mkoani Mara.
0 comments:
Post a Comment