KAMPUNI ya utalii ya Singita Grumeti Reserves (SGR), na shirika lake
dada la Grumeti Fund (GR), imetumia zaidi ya Sh milioni 16 tangu
mwanzoni mwa mwaka huu kutoa misaada ya kijamii katika maeneo mbalimbali
nchini.
Hayo yalisemwa wakati kampuni hiyo ikikabidhi msaada wa magodoro kwa
kituo cha Nyumba Salama cha mjini hapa, kinachohifadhi watoto wa kike
waliokimbia kukeketwa kutoka mikoa ya Mara na Arusha.
Akizungumza kwenye makabidhiano hayo hivi karibuni, Meneja Uhusiano
wa SGR, Ami Seki alisema huo ni mwendelezo wa kampuni kusaidia jamii
inayowazunguka katika kuunga mkono juhudi za serikali kuhudumia jamii.
“Kila mwaka kunapokuwa kunafanyika ukeketaji watoto wengi wasiotaka
kukeketwa hukimbilia kituoni hapa, ili kukabiliana na wimbi hilo ndiyo
maana kampuni ikaguswa na kuamua kutoa msaada huu wa Sh 1,375,000,”
alisema.
Meneja huyo alisema baada ya kufanya ziara kituoni hapo kuona huduma
wanazotoa , ndipo walipogundua miongoni mwa changamoto ni upungufu wa
magodoro hivyo wakaamua kuwasaidia.
Naye Janet Chapman kutoka taasisi ya Tanzania Development Trust, alisema msaada huo
Chanzo Gazeti la Habari leo
0 comments:
Post a Comment