Mkurugenzi wa Singita Grumeti Stephen Cunliffe (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk. Charles Mlingwa msaada wa madawati 500 yenye Thamani ya Tshs Milioni 112 kwa ajili ya Wilaya za Serengeti na Bunda katika hafla iliyofanyika Shule ya Msingi Makundusi Wilayani Serengeti.
Mkurugenzi wa Singita Grumeti Stephen Cunliffe (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk. Charles Mlingwa nyumba ya kuishi mwalimu yenye thamani ya Tshs Milioni 86 iliyojengwa katika Shule ya Msingi Makundusi Wilayani Serengeti.
Mkuu wa Huduma za Jamii Singta grumeti Richard Ndaskoi (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk. Charles Mlingwa msaada wa madawati 500 yenye Thamani ya Tshs Milioni 112 kwa ajili ya Wilaya za Serengeti na Bunda katika hafla iliyofanyika Shule ya Msingi Makundusi Wilayani Serengeti
Madawati yaliyotolewa na Mfuko wa Singita Grumeti kwa ajili ya Wilaya ya Bunda.
Mfuko wa Singita Grumeti umeendelea kuwa mstari wa mbele katika kuboresha hali ya elimu katika Wilaya za Serengeti na Bunda.
Hii
imedhihirika kwenye halfa ya kukabidhi madawati 500 kwa Mkuu wa Mkoa wa
Mara Dk. Charles Mlingwa ili kupunguza uhaba wa madawati katika Wilaya
hizo. Aidha Grumeti wamekabidhi nyumba ya kuishi mwalimu iliyojengwa
katika Shule ya Msingi Makundusi.
“Tuko
hapa kukabidhi madawati haya 500 yenye thamani ya Tshs Milioni 112 kwa
Wilaya za Serengeti na Bunda pamoja na nyumba hii yenye thamani ya Tshs Milioni 86” alisema Richard Ndaskoi ambae ni Mkuu wa Huduma za Jamii toka Mfuko wa Singinta Grumeti.
Akipokea
misaada hiyo, Dk. Mlingwa alisema “Nawashukuru Singita Grumeti kwa
Msaada huu wa madawati pamoja na nyumba hakika mchango wenu katika Mkoa
wa Mara unaoneka” Dk Mlingwa amewataka wawekezaji wengine katika Mkoa wa
Mara kuchangia madawati katika Wilaya za Serengeti na Bunda kwani bado
zina uhaba wa madawati.
Aidha
Dk. Mlingwa ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti kwa kuwa na
mahusiano mazuri na wawekezaji waliopo katika Wilaya hiyo “Tukiwawekea
mazingira mazuri ya kufanya shughuli zao hata wananchi pia watanufaika
na uwepo wa wawekezaji hawa” alisema Dk. Mlingwa.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu pamoja na Mkuu wa Wilaya ya
Bunda, Lydia Bupilipili wote kwa nyakati tofauti wameushukuru Mfuko wa
Singita Grumeti kwa msaada huo wa madawati na kuuomba mfuko huo
kuendelea kuchangia katika shughuli za maendeleo katika Wilaya za
Serengeti na Bunda. “Wilaya hii ina wawekezaji wengi lakini wamekuwa
nyuma katika kuchangia shughuli za maendeleo, nawapongeza kwa kuwa
mstari wa mbele kusaidia jamii inayowazunguka pamoja na kuchangia katika
maendeleo ya Wilaya ya Serengeti” alisema Nurdin Babu.
Aidha
Bi. Bupilipili ameuomba Mfuko huo kuanzisha kampeni maalumu ya kuongeza
kiwango cha ufaulu kwa watoto wa kike kwa shule za sekondari Wilayani
Bunda.
Singita
Grumeti wamekuwa wawekezaji wenye tija kwa wananchi wa Wilaya za
Serengeti na Bunda licha ya kuwa mstari wa mbele kuchangia katika
shughuli za maendeleo, kampuni hiyo pia imekuwa ikitoa ajira kwa wakazi
toka wilaya hizo mbili pamoja na kutoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi
toka wilaya hizo.
0 comments:
Post a Comment