Na. Lilian Lundo – MAELEZO - Mara
Halmashauri
tatu za Mkoa wa Mara zimevuka Lengo la Matokeo Makubwa Sasa (Big
Results Now – BRN) la asilimia 80 katika matokeo ya darasa la saba ya
mwaka 2016.
Hayo yamesemwa leo, Wilayani Tarime na Afisa Elimu wa Mkoa wa Mara Mwalimu Hamis
Lissu alipokuwa akifungua semina ya Mawasiliano na kushirikishana
jitihada zenye mafanikio kwenye Elimu kwa maafisa wa Elimu wa Mkoa wa
huo.
“Halmashauri
za Tarime Mji, Tarime Manispaa na Musoma Manispaa ni halmashauri ambazo
zimevuka lengo la BRN katika Mkoa wa Mara, Halmashauri hizo kila moja
zimepata wastani wa asilimia 82 katika matokeo ya darasa la Saba ya
mwaka, 2016,” alifafanua Lissu.
Aliendelea
kwa kusema kuwa, ufaulu wa darasa la saba katika Mkoa wa Mara umekuwa
ukipanda mwaka hadi mwaka kuanzia mwaka 2014, ambapo kwa mwaka 2014 Mkoa
wa Mara ulikuwa Mkoa wa 25 kati ya Mikoa 25, mwaka 2015 Mkoa ulishika
nafasi ya 17 kati ya Mikoa 25 na mwaka huu 2016 umeshika nafasi ya 13
kati ya Mikoa 26.
Lissu
amesema kuwa Halmashauri zote za Mkoa wa Mara zimeongeza ufaulu katika
matokeo ya mwaka huu ukilinganisha na matokeo ya mwaka 2015 na 2014.
Vile
vile amesema kuwa ongezeko hilo la ufaulu limefanikishwa kwa kiwango
kikubwa na Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania (Education Quality
Improvement Programme -Tanzania) EQUIP-T unaosimamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Uingereza.
Mpango
huo umekuwa ukitoa mafunzo ya kuboresha utendaji wa walimu darasani
pamoja na kutoa pikipiki kwa waratibu elimu kata wote ambao ndio
wafuatiliaji wakubwa wa ufundishaji wa walimu na maendeleo ya taaluma ya
mwanafunzi katika ngazi ya kata.
Aidha Lissu amesema kuwa kuna asilimia kubwa ya Mkoa huo kushika nafasi ya kumi bora kitaifa katika matokeo ya mwaka 2017.
0 comments:
Post a Comment