SHIRIKA la Mosorec International Foundation limefanikiwa kuiunganisha
wilaya ya Tarime kuwa na mahusiano na jiji la Milwaukee lililopo
Wisconsin, Marekani.
Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na shirika hilo ambalo
lipo Marekani na Tanzania ilisema uhusiano huo utaiwezesha wilaya ya
Tarime mkoani Mara kushirikiana na jiji la Milwaukee katika sekta
mbalimbali kama vile elimu, afya, kilimo, biashara utamaduni na utalii.
“Mosorec International Foundation Marekani na Tanzania imefanya kazi
ya kuunganisha haya mahusiano kwa manufaa ya wananchi wa Tarime na
Milwaukee.
Tunapenda kushukuru Serikali ya Tanzania na viongozi wake, Halmashuri
ya wilaya ya Tarime, Halmashauri ya mji wa Tarime, Mkuu wa Wilaya ya
Tarime, Glorious Luoga na Ubalozi wa Tanzania – Marekani kwa ushirikiano
wao,” alisema Mwanzilishi na Rais wa Mosorec International Foundation,
Christine Mosore katika taarifa hiyo.
Aliongeza: “Tunapenda pia kumshukuru Mwenyekiti wa Halmashauri ya
wilaya ya Tarime, Moses Misiwa kwa kufika Milwaukee, Marekani na kusaini
makubaliano hayo Novemba 7, mwaka huu.”
Hata hivyo, Mosore alisisitiza kuwa mahusiano hayo hayahusiki na masuala yoyote ya kisiasa.
Hii ni mara ya kwanza kwa wilaya ya Tarime kuwa na mahusiano ya namna
hiyo na jiji nchini Marekani. Tayari Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Wilaya ya Tarime amerejea nchini baada ya kusaini makubaliano hayo.
Chanzo Gazeti la Habari Leo
0 comments:
Post a Comment