NA HASSAN SILAYO-MAELEZO
Mkoa
wa Mara ni Moja ya Mikoa ambayo kwa kiasi kikubwa imekuwa ikiendelea na
utamaduni wa kukeketa watoto wa kike jambo ambalo ni kinyume na haki za
mtoto na sheria mbalimbali duniani.
Kila
mwaka takribani watoto milioni mbili wako katika hatari ya kukeketwa
ambako kwasasa Tanzania ina asilimia 32 ya hali ya ukeketaji suala
ambalo Serikali hairidhiki nalo.
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Bi.
Sihaba Nkinga alifanya ziara ya siku 2 Mkoani Mara katika Wilaya za
Tarime na Musoma.
Katika
ziara hiyo Bi. Sihaba ambayo alimuwakilisha Waziri wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katika
mahafali ya 9 ya Kituo cha kulea watoto waliokimbia ukeketaji cha
Masanga (ATFGM) katika kata ya Masanga Tarime Vijijini.
Katika
hotuba yake Katibu Mkuu Bi. Sihaba alionesha kushangazwa na vitendo vya
ukeketaji vinavyofanywa na wenyeji wa Mkoa wa Mara na kuviita ni
vitendo vya kikatili dhidi ya watoto wa kike, kwani inakatisha ndoto na
matarajio ya watoto hao.
Akitoa
kauli ya Serikali Bi. Sihaba alisema kuwa Serikali itawachukulia hatua
kali za kisheria watakaogundulika kuendeleza vitendo vya ukeketaji kwani
ni kinyume na Sheria ya Nchi na nikinyume na mikataba mbalimbali ya
Kimataifa iliyojielekeza katika kulinda haki mbalimbali za mtoto.
Akionesha
kudhamiria kukabiliana na tatizo la ukeketaji katika mkoa wa Mara
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto
Bi. Sihaba Nkinga alikutana na Wazee wa kimila kutoka Koo tano za
Bukenye, Nyabasi, Bukira, Butimbaru, Buhunyaga.
Katika
mazungumzo hayo yaliyolenga kuweka mikakati ya kukomesha tamaduni ya
ukeketaji mkoani Mara, Mzee wa kimila kutoka Koo ya Bukenye Mzee Elias
Maganya alisema kuwa walishapata elimu kutoka kwenye Jukwaa la Kulinda
Utu wa watoto(CDF) na changamoto ni jinsi ya kuzifikia koo nyingine
Mkoani huko ili kuwezesha kuondoa kabisa mila hiyo.
Mzee
Elias alisema kuwa sasa ni jukumu la Serikali kuona umuhimu wa
kuwawezesha kutembea Koo hadi Koo kwa ajili ya kuelimisha jamii kuhusu
madhara ya ukeketaji.
Naye
Mzee wa Kimila kutoka Koo ya Bukira Mzee Sinda Nyangore ameishauri
Serikali na mashirika mengine kutoa elimu katika vipindi vyote vya mwaka
na kuacha utaratibu wa kutoa elimu katika msimu wa ukeketaji kwenye koo
mbalimbali.
Aidha,Mzee
kutoka koo ya Butimbaru Mwita Nyasibora alishauri mpango wa kutoa elimu
kwa jamii kuhusu madhara ya ukeketaji yafanyika kwa wakati wote badala
ya kusubiri kipindi cha ukeketaji ndipo serikali na asasi nyingine za
kiraia kujitokeza kutoa elimu.
Akijibu
hoja hizo Bi. Sihaba Nkinga amesema kuwa, kweli upo umuhimu wa
kutekeleza suala hilo la kupeleka elimu juu ya madhara ya ukeketaji ili
kuweza kuwasaidia watoto wakike katika koo hadi koo kwani tofauti na
hapo lengo kusudiwa haliwezi kufikiwa na itakuwa ni tofauti na malengo
ya serikali katika kupambana na tamaduni ya ukeketaji.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tarime Bw. Glorius Luoga katika hotuba
yake aliyoitoa katika mahafali hayo, aliyataja majina ya mangariba
maarufu ambao wanatafutwa na vyombo vya dola kwa vitendo vya ukeketaji
katika maeneo mbalimbali wilayani Tarime.
Mkuu
wa Wilaya huyo pia, alisema ofisi yake imeshawapeleka katika vyombo vya
Sheria baadhi ya watu wanaojihusisha na vitendo vya ukeketaji na
kuahidi kuendelea kuwachukulia hatua kali za Kisheria wale
watakaoendelea na vitendo hivyo vya ukeketaji.
Aidha,
Bw. Luoga alioneshwa kuchukizwa na aina ya wazazi na walezi
wanaolazimisha kuwatahiri watoto wa kiume kwa mara ya pili baada ya
tohara salama kwani kitendo hicho ni sawa na kumjeruhi mtoto.
Akiongea
na wahitimu, wazazi, walezi na mangariba wastaafu, Mkuu wa Wilaya ya
Bunda Bi. Lydia Bupilipili alisema, wazazi na walezi wanapaswa kuona
umuhimu wa kuwapeleka watoto wa kike shuleni ili waweze kutimiza ndoto
walizojiwekea katika maisha yao.
Akiongea
mbele ya Mkurugenzi wa Kituo cha Kulea Watoto waliokimbia Kukeketwa cha
(ATFGM-Massanga) Sister Stella Mgaya aliishukuru Serikali ya Wilaya na
Wizara ya Afya kupitia Maafisa Maendeleo ya Jamii kwa ushirikiano
wanaoupata pale wanapohitaji.
Aidha,
Sister Stella Mgaya alisema kuwa kituo hicho kimekuwa kikikumbwa na
changamoto nyingi ikiwemo kuwa na idadi kubwa ya watoto kituoni hapo
baada wanaokataliwa na wazazi/walezi pindi wanapotoka kituoni hapo hivyo
kuongeza gharama ya kuwapeleka shuleni, Sister Mgaya
Wakisoma
risala kwa mgeni rasmi wahitimu wa kituo cha kulea watoto cha masanga
walitoa maombi yafuatayo kwa Katibu Mkuu Bi. Sihaba Nkinga waliomba
kuendelezwa kielimu pindi wanapomaliza kituoni hapo wakati mwingine
wanakataliwa na kutengwa na wazazi/walezi wao.
Aidha,
Watoto hao waliiomba pia serikali kukamata wazazi/walezi
wanaowalazimisha kukeketwa pindi wanapotoka kituoni hapo na kuendelea na
kuutilia mkazo utaratibu wa kuchukuliwa hatua kali za kisheria kwa
wazazi,walezi na mangariba wanaojihusisha na kazi ya ukeketaji ikiwemo
kifungo cha miaka 5-10 jela.
Rai
yangu kwa watanzania na hasa makabila yanayoendeleza mila ya ukeketaji
wa watoto wa kike ni kuacha tamaduni hii ambayo ni kinyume na sheria za
nchi na hata mikataba mbalimbali ya kimataifa inayolenga kumlinda mtoto
wa kike. Pia ni muda wa kujikita katika kumuendeleza mtoto wa kike
kielimu ili waweze kutimiza malengo na ndoto walizojiwekea kwani
“Tanzania Bila ukeketaji inawezekana”
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment