Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi akikagua
mfumo wa kodi wa Manispaa ya Musoma Mkoani Mara. Kushoto kwake Afirsa
Ardhi wa Manispaa hiyo Ndugu Joseph Kamonga akimuonesha mfumo wa kodi
unavyofanya kazi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi akizindua Mpango Kabambe (Master Plan) Manispaa ya Musoma Mkoani Mara.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi akikambidhi Mpango Kabambe wa Manispaa ya Musoma Meya wa Manispaa ya hiyo Mh. Patrick Gumbo.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi akiongea na viongozi na wananchi wa Manispaa ya Musoma katika uzinduzi wa Mpango Kabambe wa Manispaa hiyo.
Na. Hassan Mabuye
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi akizindua Mpango Kabambe (Master Plan) Manispaa ya Musoma Mkoani Mara.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi akikambidhi Mpango Kabambe wa Manispaa ya Musoma Meya wa Manispaa ya hiyo Mh. Patrick Gumbo.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi akiongea na viongozi na wananchi wa Manispaa ya Musoma katika uzinduzi wa Mpango Kabambe wa Manispaa hiyo.
Baadhi
ya Wananchi na Watendaji wa Manispaa ya Musoma wakimsikiliza Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi katika uzinduzi
wa Mpango Kabambe wa Manispaa hiyo mkoani mara.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi amefanya
ukaguzi wa mfumo wa kodi ya ardhi katika manispaa ya Musoma Mjini mkoa
wa Mara ambapo amebaini wananchi 231 wanadaiwa Kodi ya Pango la Ardhi
kiasi cha shilingi milioni 271.
Mhe
Lukuvi amemtaka Afisa Ardhi wa manispaa ya Musoma bwana Joseph Kamonga
kuwasilisha majina ya wadaiwa hao katika Mahakama ili waweze kuchukuliwa
hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kupiga mnada majengo na mali zao
kawa wakikaidi kulipa kodi hiyo.
“nimeagiza
kesi za madai ya kodi zitolewe hukumu ndani ya siku moja tu ili wadaiwa
waweze kuchukuliwa hatua ya kuuzwa kwa mali zao haraka” Mhe Lukuvi
aliyasema hayo wakati alipo fanya ziara ya kukagua mfumo wa kodi wa
manispaa ya Musoma mjini ili kuhakikisha wamiliki wote wa ardhi nchini
wanalipa kodi kwa hiari kabla ya hatua za kisheria hazijafuata dhidi
yao.
Aidha,
Waziri Lukuvi amefanya uzinduzi wa mpango kabambe (Master Plan) wa
Manispaa ya Musoma na kuwapongeza viongozi na watendaji wa manispaa ya
Musoma kwa kuwa manispaa ya kwanza nchini kuweza kuzindua mpango kabambe
wa mji wao. Pia aliwapongeza kwa uzalendo wao wa kutumia kampuni za
ndani katika utekelezaji wa mpango huo.
Manispaa
ya Musoma ilitoa tenda kwa kampuni zalendo ijulikanayo kama CRM ambayo
ilithibitisha uzalendo wake kwa kumaliza kazi waliyopewa kwa wakati.
Kutokana na hilo, Mheshimiwa Waziri alizitaka manispaa zingine kutumia
kampuni za ndani ya nchi ambazo zimesajiliwa na wizara.
Mbali
na hayo, Mh. Lukuvi aliiagiza manispaa ya Musoma kuandaa mpango mkakati
wa utekelezaji wa mpango kabambe kwa kutumia wataalam wao (wa serikali)
au Makampuni ya ndani. Pia, aliiagiza manispaa ya Musoma kutoa nakala
za kutosha ili mpango huo uwafikie wadau wote, na kutaka mpango huo
utafsiriwe kwa Kiswahili ili madiwani na wenyeviti wa serikali za mitaa
waweze kuwafikishia wananchi kwa urahisi.
Maagizo
mengine ni pamoja na kwataka viongozi wa manispaa zote nchini kusimamia
suala la ujenzi unaofuata mipango miji na kupiga marufuku wananchi
wanaojenga bila kupewa vibali vya ujenzi katika maeneo ambayo
yamekamilisha mipango kabambe na kuagiza nyumba itakayojengwa bila
kibali ivunjwe.
Pia
aliwataka maafisa ardhi wa manispaa kutoa elimu ya masuala ya Ardhi kwa
kwa maafisa watendaji wa Mitaa ili elimu na utekelezaji wa masuala ya
ardhi ngazi ya wananchi uwe ni kwa urahisi na wenye kueleweka.
Na. Hassan Mabuye
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
0 comments:
Post a Comment