PROF. MBARAWA ATOA MIEZI 9 KWA MKANDARASI NYAZA ROADS WORKS

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na wakazi wa kijiji cha Kisorya, wilaya ya Bunda alipokutana nao baada ya kukagua ujenzi wa barabara ya Bulamba-Kisorya yenye urefu wa KM 51 inayojengwa kwa kiwango cha lami, wilayani humo, mkoani Mara.
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima, akisisitiza jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, katika ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya Bulamba-Kisorya yenye urefu wa KM 51 inayojengwa kwa kiwango cha lami, wilayani Bunda, mkoani Mara.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Kangi Lugola, ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mwibara, akiteta jambo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, wakati wa ukaguzi wa barabara ya Bulamba-Kisorya yenye urefu wa KM 51 inayojengwa kwa kiwango cha lami, wilayani Bunda, mkoani Mara.
Muonekano wa sehemu ya barabara ya Bulamba-Kisorya yenye urefu wa KM 51 inayojengwa kwa kiwango cha lami, wilayani Bunda, mkoani Mara.
Muonekano wa sehemu ya barabara ya Makutano-Sanzate yenye urefu wa KM 50 inayojengwa kwa kiwango cha lami ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 54. Barabara hiyo inajengwa na wakandarasi wazawa M/S Mbutu JV.

…………………

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemtaka mkandarasi Nyanza Road Works kukamilisha ujenzi wa barabara ya Bulamba-Kisorya yenye urefu wa KM 51 kwa kiwango cha lami ifikapo mwezi Novemba mwaka huu.

Prof. Mbarawa ametoa kauli hiyo wakati akikagua ujenzi wa barabara hiyo na kuzungumza na wananchi wa kijiji cha Kisorya na kusema kuwa usanifu wa barabara na madaraja katika barabara hiyo umewasilishwa sasa ni jukumu la mkandarasi kuendelea na ujenzi kwa kasi na kwa viwango vya ubora.

“Serikali ina nia njema kwa wananchi wa wilaya ya Bunda na mkoa wa Mara sasa tunaijenga barabara hii na mwishon mwa mwaka mtaanza kunufaika nayo”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Ameongeza kuwa kukamilika kwa barabara hiyo utarahisisha mawasiliano na kupunguza gharama za shughuli za usafirishaji wa samaki, mazao na abiria, uboreshaji makazi na kukuza uchumi kwa maeneo yaliyo kando ya barabara.

Kuhusu suala la fidia, Prof. Mbarawa amefafanua kuwa Serikali italipa fidia kwa mwananchi ambaye barabara imemfuata kama anavyostahili.

“Serikali haina nia ya kumuonea mtu yeyote bali inachofanya inalipa kulingana na sheria inavyoelekeza”, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.

Katika hatua nyingine Waziri Prof. Mbarawa amekagua ujenzi wa barabara ya Makutano-Sanzale KM 50 na kumwagiza mkandarasi wa M/S Mbutu JV Contractor (T) kuhakikisha wanakamilisha mradi huo kabla ya mwezi Julai mwaka huu.

“Mradi huu ni wa muda mrefu sana na wananchi wameusubiri kwa muda kama hamtamaliza mradi huu mpaka mwezi juni, hii itakuwa kazi yenu ya mwisho, maana ninategemea nyinyi kama wazawa mngekuwa wa mfano” amesisitiza Prof. Mbarawa.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima amesema kwa sasa mkoa umeamua kupata taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa miradi ya barabara kila baada ya miezi mitatu ili kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati.

Naye Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Mara, Mhandisi Mlima Ngaile amesema Wakala utasimamia mradi wa ujenzi wa barabara hizo na kuhakikisha mradi unazingatia viwango kulingana na mkataba.

Waziri Prof. Mbarawa yuko mkoani Mara kwa ziara ya siku mbili akiwa na lengo la kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya sekta ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano.

Kamishna wa TRA amsimamisha kazi Meneja wa Mara

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),  Charles Kichere amemsimamisha kazi Meneja wa TRA Mkoa wa Mara  Nicodemus Mwakilembe kwa kushindwa kusimamia vizuri mashine za  Kielektroniki za Kutolea Risiti (EFDs).

Uamuzi huo umetokana na ziara ya kushtukiza ya kukagua matumizi ya EFD aliyoifanya Kamshina Mkuu wa Tra kwenye baadhi ya maduka ya biashara Wilayani Bunda Mkoa wa Mara.

Akizungumza mara baada ya ziara yake, Kamishna Mkuu Kichere alisema kuna wafanyabishara wengi mkoani Mara  ambao walishalipa fedha kwa ajili ya kupata mashine za EFD lakini mpaka sasa hawajapatiwa mashine hizo.

"Katika ziara yangu nimegundua kwamba, wapo wafanyabiashara ambao wameshalipia mashine tangu mwaka 2013, 2014 na 2015 lakini mpaka sasa bado hawajapatiwa mashine za EFD na wamekuwa wakitumia mwanya huo kama kinga ya kutochukuliwa adhabu na TRA wakati Meneja wa Mkoa  yupo na hachukui hatua zozote. Huu ni uzembe uliopitiliza na kamwe siwezi kuuvumilia," amesema  Kichere.


Kichere amewaagiza mameneja wote wa TRA nchi nzima pamoja na majukumu mengine, kuhakikisha wanasimamia kikamilifu matumizi ya mashine za EFD katika mikoa yao na amesema hatasita kumuwajibisha meneja yeyote atakayeshindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

Ziara hiyo ya kushtukiza imewawezesha wafanyabiashara waliokuwa wamelipia mashine za EFD miaka ya nyuma, kupata mashine hizo na kufundishwa jinsi ya kuzitumia ambapo wengine wamejitokeza kununua mashine hizo kwa ajili ya biashara zao.

Kamishna  Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania yuko mkoani Mara kwa ziara ya siku tano  ambapo amepata nafasi ya kutembelea Vituo vya Forodha mipakani na ofisi mbalimbali za mamlaka hiyo pamoja na baadhi ya wafanyabiashara akikagua matumizi ya mashine za EFD.

KAMISHNA MKUU WA TRA AMSIMAMISHA KAZI MENEJA WA TRA MKOA WA MARA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (aliyekaa mbele) akiongea na kutoa maagizo kwa Meneja wa TRA Wilaya ya Bunda Mkoani Mara pamoja na wafanyakazi wengine wa Mamlaka hiyo kuhusu ukusanyaji wa mapato ya Serikali mara alipotembelea ofisi ya TRA Wilayani hapo ili kujionea namna ukusanyaji mapato unavyofanyika mapema 3 Februari, 2018.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (kulia) akimsisitizia jambo Mfanyabiashara wa duka la nguo Wilayani Bunda Mkoani Mara kuhusu suala la umuhimu wa kutumia mashine ya Kielektroniki ya Kutolea Risiti (EFD) mara alipofanya ukaguzi wa mashine hizo katika baadhi ya maduka Wilayani hapo 3 Februari, 2018.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (kulia) akikagua taarifa ya mauzo ya siku ya Mashine ya Kielektroniki ya Kutolea Risiti (EFD) toka kwa Wafanyabiashara wa duka la vifaa vya nyumbani Wilayani Bunda Mkoani Mara mara alipofanya ukaguzi wa mashine hizo katika baadhi ya maduka Wilayani hapo 3 Februari, 2018.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa TRA Wilaya ya Bunda Mkoani Mara pamoja na wafanyakazi wengine wa Mamlaka hiyo mara alipotembelea ofisi ya TRA Wilayani hapo ili kujionea namna ukusanyaji mapato unavyofanyika mapema 3 Februari, 2018.(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-TRA).



Na: Veronica Kazimoto-Bunda, 

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere amemsimamisha kazi Meneja wa TRA Mkoa wa Mara Ndg. Nicodemus Mwakilembe kutokana na uzembe wa kutosimamia vizuri matumizi ya Mashine za Kielektroniki za Kutolea Risiti (EFDs) kwa wafanyabiashara wa mkoani kwake. 

Uamuzi huo umetokana na ziara ya kushtukiza ya kukagua matumizi ya EFD aliyoifanya Kamshina Mkuu wa TRA kwenye baadhi ya maduka ya biashara Wilayani Bunda Mkoa wa Mara. Akizungumza mara baada ya ziara yake, Kamishna Mkuu Kichere alisema Meneja huyo ameonyesha uzembe wa hali ya juu kwani kuna wafanyabishara wengi mkoani kwake ambao walishalipa fedha kwa ajili ya kupata mashine za EFD lakini mpaka sasa hawajapatiwa mashine hizo. 

"Katika ziara yangu nimegundua kwamba, wapo wafanyabiashara ambao walikwisha kulipia mashine tangu mwaka 2013, 2014 na 2015 lakini mpaka sasa bado hawajapatiwa mashine za EFD na wamekuwa wakitumia mwanya huo kama kinga ya kutochukuliwa adhabu na TRA wakati Meneja wa Mkoa yupo na hachukui hatua zozote. Huu ni uzembe uliopitiliza na kamwe siwezi kuuvumilia," alisema Kichere. 

Kutokana na uzembe huo, Kamishna Mkuu Kichere amewaagiza Mameneja wote wa TRA nchi nzima pamoja na majukumu mengine, kuhakikisha wanasimamia kikamilifu matumizi ya mashine za EFD katika mikoa yao na amesema hatasita kumuwajibisha Meneja yeyote atakayeshindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo. 

Ziara hiyo ya kushtukiza imewawezesha wafanyabiashara waliokuwa wamelipia mashine za EFD miaka ya nyuma, kupata mashine hizo na kufundishwa jinsi ya kuzitumia ambapo wengine wamejitokeza kununua mashine hizo kwa ajili ya biashara zao. Kamishna Mkuu aliongeza kuwa, mashine za EFD zina umuhimu sio tu kwa Serikali kupata mapato bali kwa wafanyabiashara husika kwani huwawezesha kutunza kumbukumbu, kujua mwenendo halisi wa biashara zao na hatimaye kulipa kodi stahiki. 

Sambamba na hayo, Kichere amewataka wananchi wasiishie tu kudai risiti bali wakishachukua risiti hizo wazikague ili kuthibitisha uhalali wake na usahihi wa kiasi cha pesa walicholipa. Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania yuko mkoani Mara kwa ziara ya siku 5 ambapo amepata nafasi ya kutembelea Vituo vya Forodha mipakani na ofisi mbalimbali za mamlaka hiyo pamoja na baadhi ya wafanyabiashara akikagua matumizi ya mashine za EFD.

SHIRIKA LA AGPAHI YAKABIDHI KOMPYUTA 46 KWA AJILI YA VITUO VYA TIBA NA MATUNZO KWA WATU WANAOISHI NA VVU MKOA WA MARA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Shirika la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) limekabidhi kompyuta 46 zenye thamani ya shilingi milioni 70.2 zitakazotumika katika vituo vya tiba na matunzo (CTC) kwa watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU) kwenye halmashauri za wilaya mkoani Mara.
Shirika hilo limekabidhi kompyuta hizo siku ya Jumatatu, Januari 22, 2018 kwa Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mara, Raphael Nyanda katika ukumbi wa mikutano wa Mwembeni uliopo katika Manispaa ya Musoma.
Akizungumza wakati wa kukabidhi kompyuta hizo, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa alisema kompyuta hizo zitatumika kuhifadhi takwimu za wateja katika vituo vya tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU na kusaidia upatikanaji wa taarifa kwa haraka na kwa usahihi zaidi.

“Leo tunayo furaha kukabidhi kompyuta 19 ambayo ni nyongeza ya kompyuta 27 ambazo zimeshapelekwa kwenye vituo vya afya hivyo hadi sasa tutakuwa tumekabidhi jumla ya kompyuta 46 tulizokabidhi kwa kipindi cha mwaka mmoja tangu tuanze kutekeleza miradi ya Ukimwi katika mkoa wa Mara”, alieleza Dk. Sekela.
“Mbali na kukabidhi kompyuta pia tumefanikisha ajira kwa makarani takwimu "Data Clerks" 84 kwa halmashauri zote na tunawezesha upatikanaji wa mtandao wa intaneti kwa kutoa modem ili kurahisisha uingizaji wa takwimu katika mfumo wa kielektroniki na kutoa taarifa kwa wakati stahiki”,aliongeza Dk. Sekela.
Katika hatua nyingine alisema shirika hilo linatekeleza miradi ya Ukimwi katika vituo 112 vya kutolea huduma za afya mkoani Mara, kati ya vituo hivyo 67 ni vituo vya kutolea tiba na matunzo na 46 ni vya kutolea huduma ya kupunguza maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT).
Dk. Sekela alibainisha kuwa katika kipindi cha mwezi Oktoba 2016 hadi Septemba 2017, jumla ya watu 182,712 mkoani humo walipata huduma ya upimaji wa VVU, kati yao wanaume walikuwa 51,868 (28%), watoto 31,423 (17%). Kati ya watu 182,712 waliopima, 7,325 (4%) waligundulika kuwa na maambuzi ya VVU na 6,022 (82%) walianzishiwa dawa za kupunguza makali ya VVU. 
Aliongeza kuwa katika kipindi hicho pia akina mama wajawazito 49,937 walipima VVU , kati yao 981 sawa na 2% waligundulika kuwa na maambukizi ya VVU na 755 sawa na 77% walianzishiwa dawa za kupunguza makali ya VVU.
Akipokea kompyuta hizo, Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mara, Raphael Nyanda alilishukuru shirika la AGPAHI kwa kutoa msaada huo na kuzitaka halmashauri za wilaya kuzitunza ili zidumu.

“Tunawashukuru sana AGPAHI na Watu wa Marekani kwa kuendelea kutushika mkono katika sekta afya, mwaka huu mmetuongeza shilingi bilioni 7.2 kwenye bajeti ya mkoa kwa ajili ya masuala ya Ukimwi, kwa kweli mmekuwa wadau wakubwa wa afya, naomba tuendelee kushirikiana kuwahudumia wananchi”, alieleza Nyanda.

“Serikali ya mkoa itasimamia vizuri fedha hizi,wakurugenzi tumieni fedha za wafadhili kwa malengo yaliyokusudiwa, msihamishe fedha, pia tuache tabia ya kufanya kazi kwa mazoea na watendaji hakikisheni mnatoa takwimu sahihi", alisema Nyanda.
Mbali na kukabidhi kompyuta, Shirika la AGPAHI pia linaendesha mafunzo ya siku mbili kuhusu taratibu na kanuni za matumizi ya fedha za wafadhili ambao ni Watu wa Marekani kupitia Centres for Disease Control (CDC) yaliyohudhuriwa na wakurugenzi na viongozi wa timu za afya za mikoa na wilaya.
Wakurugenzi wa halmashauri za wilaya wanaojengewa uwezo ni kutoka Mji wa Bunda,Tarime Mji, Manispaa ya Musoma, Bunda Vijijini, Butiama, Musoma Vijijini, Rorya,Tarime na Serengeti na timu za afya za mkoa na wilaya kuhusu namna ya kutumia fedha za mfadhili sawa sawa na matakwa na makubaliano kati ya AGPAHI na serikali ya Marekani.
Mwaka huu shirika limetoa shilingi bilioni 7.2 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya Ukimwi mkoani Mara ikiwa ni mara sita zaidi ya fedha iliyotolewa na shirika hilo mwaka 2016/2017 ambayo ilikuwa shilingi bilioni 1.1.
Shirika la AGPAHI linatekeleza miradi ya Ukimwi katika mikoa sita nchini ambayo ni Shinyanga, Simiyu, Geita,Mwanza, Tanga na Mara likishirikiana na serikali ya Tanzania kwa ufadhili wa serikali ya Watu wa Marekani kupitia CDC katika kutekeleza mradi wa “Boresha” ambao unatoa huduma za kinga, tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU na Ukimwi.


Mgeni rasmi, Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mara, Raphael Nyanda akizungumza wakati wa zoezi la makabidhiano ya kompyuta na kufungua mafunzo ya taratibu na kanuni za matumizi ya fedha za wafadhili katika ukumbi wa mikutano wa Mwembeni manispaa ya Musoma.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mara, Raphael Nyanda akilishukuru shirika la AGPAHI kwa kuipatia serikali ya mkoa wa Mara shilingi bilioni 7.2 kwa ajili ya miradi ya Ukimwi.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa akizungumza wakati wa kukabidhi kompyuta 46. Kushoto ni Meneja wa Shirika la AGPAHI Kanda ya Ziwa, Dk. Nkingwa Mabelele. Kulia ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mara, Raphael Nyanda.
Dk. Sekela alisema kompyuta hizo zitatumika kuhifadhi takwimu za wateja wa CTC katika vituo vya afya na kusaidia upatikanaji wa taarifa kwa haraka na kwa usahihi zaidi.
Dk. Sekela akizungumza wakati wa kukabidhi kompyuta hizo.
Mganga Mkuu wa mkoa wa Mara, Dk. Francis Mwanisi akilishukuru shirika la AGPAHI kwa msaada wa kompyuta 46.
Maboksi yenye kompyuta zilizotolewa na shirika la AGPAHI kabla ya kukabidhiwa kwa wakurugenzi wa halmashauri za wilaya mkoani Mara.
Katikati ni Dk. Sekela akionyesha moja kati ya kompyuta 46 zilizotolewa na shirika la AGPAHI. 
Dk. Sekela akielezea zaidi kuhusu kompyuta hizo.
Dk. Sekela na Kaimu Katibu Tawala, Raphael Nyanda wakikabidhi kompyuta kwa Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Rorya Charles Kitamuru Chacha (aliyevaa nguo nyeusi kushoto) aliyeambatana na timu ya afya ya halmashauri hiyo.
Makabidhiano kwa viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Butiama yakiendelea.
Viongozi wa halmashauri ya Manispaa ya Musoma wakiongozwa na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Fidelica Myovela (aliyeshika boksi la kompyuta) wakipokea kompyuta.
Zoezi la makabidhiano ya kompyuta likiendelea.
Viongozi wa timu za afya za mikoa na wilaya wakiwa ukumbini.
Mratibu wa AGPAHI mkoa wa Mara, Alio Hussein akielezea lengo la mafunzo ya taratibu na kanuni za matumizi ya fedha za wafadhili ambao ni Watu wa Marekani kupitia Centres for Disease Control (CDC).
Alio Hussein alisema shirika hilo linatekeleza miradi ya Ukimwi kwenye halmashauri 9 za wilaya mkoani Mara.
Afisa Ruzuku Mwandamizi wa shirika la AGPAHI, Leticia Gilba akitoa mada kuhusu vigezo na masharti ya mkataba wa utekelezaji wa Mradi wa Boresha mkoani Mara unaofadhiliwa na Watu wa Marekani kupitia CDC.
Leticia Gilba akiendelea kutoa mada ukumbini. 
Leticia Gilba akielezea kuhusu sheria na taratibu za matumizi ya fedha za wafadhili.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Rorya, Charles Kitamuru Chacha akichangia mada wakati wa mafunzo hayo.
Mratibu wa Ukimwi wa halmashauri ya wilaya ya Musoma, Mwanaidi Francis akichangia hoja wakati wa majadiliano ukumbini.
Kaimu Mganga Mfawidhi hospitali teule ya wilaya ya Rorya, Dk. Baraka Malegesi akichangia hoja wakati wa mafunzo hayo.
Picha ya pamoja - wafanyakazi wa AGPAHI, wakurugenzi wa halmashauri za wilaya na timu za afya za mkoa na wilaya. 
Picha ya pamoja.
 
CREDIT:MALUNDE BLOG

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMTEMBELEA MAMA MARIA NYERERE NA KUTOA HESHIMA KWENYE KABURI LA BABA WA TAIFA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakizungumza na Mama Maria Nyerere wakati walipomtembelea nyumbani kwake Mwitongo, Butiama Januari 20, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiongozana na Mama Maria Nyerere kuingia kwenye uwanja wa Mwenge katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu katika kijiji cha Butiama Januari 20, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mama Maria Nyerere wakati alipomtembelea nyumbani kwake Mwitongo, Butiama Januari 20, 2018. Kulia ni mkewe Mary .
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akiwasha mshumaa kwenye kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere eneo la Mwitongo, Butiama, Januari 2018. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima na kushoto ni mkewe Naima .
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiweka shada la maua kwenye kaburi la Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere eneo la Mwitongo, Butiama Januari 20, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa , Mkewe Mary na Mama Maria Nyerere wakiwapungia wananchi katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika uwanja wa Mwenge kijijini Butiama Januari 20, 2018
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Mwenge katika kijiji cha Butiama Januari 20, 2017
Wananchi wa Butiama wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Mwenge katika kijijini hapo Januari 2018
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Butiama katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye uwanja wa Mwengekijijini hapo Januari 20, 2018.
Mama Maria Nyerere akiwasalimia wananchi wa Butiama katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye uwanja wa Mwenge kijijini hapo Januari 20, 2018.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa