Home » » ASANTENI NA KWAHERINI HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA

ASANTENI NA KWAHERINI HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru, 2024 ndugu Godfrey Eliakimu Mnzava siku ya tarehe 3/8/2024 aliwashukuru Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kwa mapokezi mazuri waliyoyapata.

Ndugu Mnzava alikiri kupokea taarifa kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mh Dkt Vicent Anney kuhusiana na mkesha wa Mbio za Mwenge, na shughuli zote zilizofanyika wakati wa mkesha.

Pia, alishauri wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kuhakikisha wanapima afya zao mara kwa mara na kuwa na mazoea ya kufanya mazoezi kwa ajili ya kulinda afya zao.

TUNZA MAZINGIRA NA SHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA TAIFA ENDELEVU.


0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa